Sheikh Naim Qassim huku akitilia mkazo kuhusu misimamo ya Hizbullah kuhusu kumchagua Rais mpya wa Lebabon ametahadharisha kuhusu kuingia madarakani shakhsia mtiifu na kibaraka wa Marekani na kusema: Hizbullah inaheshimu na kufungamana na suala la kuendesha uchaguzi wa rais kama ilivyopangwa.
Sheikh Qassim ameongeza kuwa: Rais mpya wa Lebanon ni lazima azingatie kanuni ya dhahabu yaani muqawama, jeshi na wananchi ambayo inalinda taifa na maliasili zake na pia izza na kujitawala kwa Lebanon. Bunge la Lebanon limeahirisha uchaguzi wa rais wa nchi hiyo hadi Alhamisi wiki hii
Bunge la Lebanon limeahirisha zoezi la kumchagua rais wa nchi hiyo hadi Alhamisi kutokana na kukosekana kwa akidi inayohitajika bungeni. Wagombea wa kiti cha rais wanahitajia kupata theluthi mbili ya kura za ndio za wabunge 128 wa Lebanon katika duru ya kwanza ya upigaji kura. Inafaa kuashiria hapa kuwa, duru ya miaka sita ya Rais Michel Aoun inamalizika tarehe 31 mwezi huu wa Oktoba na kwa sababu hiyo wanasiasa wa Lebanon wamebainisha wasiwasi wao kuhusu ombwe linaloweza kujitokeza kwa kusalia tupu nafasi hiyo ya rais wa nchi.
342/